Tusichukue sheria mkononi

Taifa Leo - - BARUA -

WANAUME wanahitaji mafunzo kuhusu maisha ili wakome kutumia nguvu kusuluhisha changamoto zao za kinyumbani.

Hivi majuzi kisa kilitokea ambapo mwanamume alimuua mwanamume mwenzake kwa madai eti aliwapata na mkewe chumbani. Visa hivi vinazidi kuongezeka katika jamii humu nchini.

Mshukiwa huyo anafaa kuchukuliwa hatua kwani alichukua sheria mikononi mwake na kusababisha kifo cha mwenzake. Badala ya kutenda mauaji hayo, wangekaa chini na wasikizane na mkewe pamoja na mwanaume huyo.

MARGARET KIMANI, Shule ya Upili ya Gachoka, Gatundu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.