Kenya yafufua mazungumzo kuhusu mkataba ya kibiashara kati ya EU na EAC

Taifa Leo - - RIZIKI HABARI ZA KILIMO NA BIASHARA - FAUSTINE NGILA

KENYA imeanzisha majadiliano mapya kuhusu kutekelezwa kwa makubalino ya kibiashara yaliyokwama baina ya Muungano wa Ulaya (EU) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) huku ikihofia huenda ikazuiwa kuuza bidhaa zake katika soko kuu la muungano huo.

Makubaliano hayo mapya yanalenga kuondoa ushuru unaotozwa bidhaa za mataifa ya EAC kwenye soko la EU.

Mataifa ya Kenya na Rwanda yalitia saini makubaliano hayo mwaka uliopita, lakini yanahitaji kupata saini ya kila taifa mwanachama wa EAC ili kurasimishwa.

“Tumekuwa na mikutano na wawakilishi wa EU Jumatano na Alhamisi na tunajizatiti kuboresha kanda yetu lakini uamuzi wa mwisho utatolewa na EU kuhusu kitakachofanyika iwapo mataifa mengine ya EAC yatakataa makubaliano hayo,” akasema Waziri wa Uchumi na Biashara Bw Adan Mohamed.

Waziri huyo alisema kuwa kuna matumaini Kenya itaendelea kuuza bidhaa zake katika soko la Ulaya chini ya makubaliano ya awali hata ikiwa EU haitakubali makubaliano Kenya inataka.

Hapo Machi mwaka huu, Kenya iliishutumu Tanzania na Uganda kwa kukataa kutia saini makubaliano hayo licha ya mataifa mengine wanachama kufanya hiyo.

Bw Mohamed amesema kwamba, msimamo wa mataifa hayo mawili eti makubalino hayo yataumiza biashara za nyumbani, yameshughulikiwa katika makubaliano mapya.

Iwapo Kenya itafungiwa nje, itapoteza uwezo wake wa kuuza bidhaa katika soko la EU, hali itakayopandisha ushuru inayotozwa kwa mauzo ya nje kwa zaidi ya Sh100 milioni kila wiki, kama ilivyokuwa mwaka 2014.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.