KWS yafanikiwa kunasa, kusafirisha ndovu 6 walioishi kwa shamba la mtu binafsi kwa miezi 4

Taifa Leo - - RIZIKI HABARI ZA KILIMO NA BIASHARA -

MAAFISA wa Shirika la Uhifadhi wa Wanyama pori (KWS), Alhamisi walifanikiwa kuwasafirisha ndovu sita, baada ya kuishi kwenye shamba la mmiliki binafsi kwa zaidi ya miezi minne.

Ndovu hao ambao wanasemekana kuhamia kwenye maeneo ya Kambi ya Moto, Kaunti ya Baringo waliwekwa kwenye hifadhi ya shamba la Chemeron baada ya malalamishi kutoka kwa wakazi kuwa waliharibu mimea yao walipofika humo mnamo Juni.

Wanyama hao walirejeshwa kwenye mbuga ya Milima ya Aberdare wanakodaiwa kutoroka katika kile maafisa wa KWS walichokitaja kuwa kuhama kwa kawaida kulingana na misimu.

Akiongoza operesheni ya kudhibiti Wanyama hao, Naibu Mkurugenzi wa eneo la uhifadhi la Central Ril Bw Aggrey Maumo alisema waliamua kuwahamisha Wanyama hao kuwapeleka kwa makazi bora ili wawe wakiwafuatilia kwa karibu.

Na Peter Mburu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.