Matangazo 2OOO yalitayarishwa na shirika la habari Urusi- Twitter

Mtandao wafichua RT ilitumia Sh27m kwa matangazo kwa lengo la kushawishi kura Amerika

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA - Na AFP

MTANDAO wa Twitter Alhamisi ulifichua kuwa karibu matangazo 2,000 yaliyotayarishwa na shirika la habari la Urusi, yalichapishwa na mtandao huo mnamo 2016 hatua ambayo inashukiwa kujaribu kushawishi uchaguzi mkuu uliopita nchini Amerika.

Shirika hilo linasemekana kufanya hivyo kwa lengo la kuvuruga uchaguzi wa urais nchini Amerika.

Taarifa ya Twitter ilisema kampuni hiyo ilitoa habari kwa wachunguzi kuhusiana na matangazo hayo ya RT, runinga iliyo na ushirika na serikali ya Urusi.

Twitter ilisema RT ilitumia takriban Sh27 milioni kuweka matangazo hayo ambayo huenda yalikuwa na lengo la kushawishi uchaguzi wa Amerika.

Ilisema hayo baada ya Facebook kukubali kuwa mashirika ya mataifa ya kigeni ikiwemo na Urusi yalilipa kuweka matangazo ya kisiasa katika mtandao huo wa kijamii, na kukiuka sheria za uchaguzi za Amerika.

Habari iliyowekwa katika blogu na Twitter ilisema makamu wa rais anayesimamia sera za umma Colin Crowell alikutana na wafanyakazi kutoka mashirika mawili ya uchunguzi yanayochunguza kisa hicho Alhamisi.

“Ni shughuli inayoendelea na tutaendelea kushirikiana na wachunguzi,” ilisema taarifa hiyo.

Twitter ilisema ilichunguza jitihada za maajenti wa kimataifa kuingilia uchaguzi wa Amerika baada ya Facebook kuashiria kuwa ilipata akaunti 450 ambazo ziliaminika kutumiwa kwa shughuli hiyo.

“Kati ya akaunti 450 ambazo zilitolewa na Facebook katika uchunguzi huo, tulifikia uamuzi kuwa akaunti 22 zimeshirikishwa moja kwa moja Twitter,” ilisema taarifa hiyo.

“Akaunti zilizobainishwa zilisimamishwa mara moja kwa kukiuka kanuni na sheria za Twitter hasa kanuni ya kutuma Ripoti ya Twitter jumbe kwa watu zaidi safari moja,” ilisema taarifa.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa RT, ambayo ilitajwa Januari katika ripoti za uchunguzi wa Amerika kuhusiana na kuingiliwa kwa uchaguzi wa Amerika, ilitumia Sh27 milioni mwaka wa 2016 kwa matangazo 1,823 Twitter ambayo yalilenga soko la Amerika.

“Kampeni hizo zilikuwa zikilenga wanaofuata mashirika makuu ya habari na kukuza matangazo hayo ya RT katika taarifa za habari,” iliongeza taarifa hiyo.

“Kati ya akaunti 45O ambazo zilitolewa na Facebook katika uchunguzi huo, tulifikia uamuzi kuwa akaunti 22 zimeshirikishwa na Twitter.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.