Rais alia vikwazo vya Amerika vimefanya taifa lake lidhoofike

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

RAIS wa Sudan Omar al-bashir, Alhamisi alisema kuwa vikwazo vya Amerika dhidi ya taifa hilo vimeidhoofisha taifa hilo na kuwafanya raia wake kupitia magumu.

Alisema hayo wiki mbili kabla ya Rais Donald Trump kuamua ikiwa ataiondolea vikwazo hivyo kabisa.

Vikwazo hivyo viliwekwa miongo miwili iliyopita kutokana na madai ya serikali kuunga mkono makundi ya Kiislamu.

“Vikwazo hivyo vilivyowekewa nchi yetu tangu 1997 vimedhoofisha nchi yetu na taasisi, na kuwafanya wananchi kupitia hali ngumu sana,” alisema Bashir wakati wa mkutano wa kiusalama na uchunguzi Afrika uliofanyika Khartoum.

“Licha ya vikwazo, jitihada inafanywa kuimarisha usalama nchini na udhibiti katika kukabiliana na makundi ya wanamgambo.”

Vikwazo hivyo vimesababisha Sudan kutokuwa na uwezo wa kupata ufadhili wa kifedha kutoka kwa benki za kimataifa. Pia lazima itimize kanuni nyingi kabla ya kuhusika katika biashara ya kimataifa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.