22 wafa kufuatia msukumano wa abiria katika daraja la reli

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

WATU 22 waliaga dunia Ijumaa asubuhi katika daraja la reli mjini Mumbai, abiria walipoangukiana na kukanyagana.

Ajali hiyo ilitokana na kuwa watu wengi waliokuwa wamejikinga mvua iliyoanza kunyesha ghafla chini ya daraja hilo.

Ilitokea watu walipoanza kutoka chini ya daraja hilo safari moja, alisema msemaji wa Shirika la Reli la India Anil Saxena.

Avinash Supe, msimamizi wa wanafunzi katika Hospitali ya KEM, aliambia AFP kuwa watu 22 walikufa.

Daraja hilo linaunganisha vituo vya safari za garimoshi vya Elphinstone na Parel kusini mwa Mumbai.

Idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, alisema msemaji wa shirika la kudhibiti majanga eneo hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.