Ndoa za kwanza za jinsia moja zahalishwa

Taifa Leo - - HABARI ZA AFRIKA NA DUNIA -

WAPENZI wa jinsia moja nchini Ujerumani watafunga ndoa kwa mara ya kwanza kesho Jumapili baada ya miaka mingi ya kufanya kampeni kuruhusu ndoa za mashoga nchini humo.

Sasa, mashoga watakuwa na uhuru wa kubadilisha uhusiano wao wa kimapenzi kwa mara ya kwanza mjini Berlin.

Harusi zaidi zitafanywa kesho katika miji ya Hanover, Hamburg na kwingineko.

Serikali iliruhusu ndoa hizo kuhalalishwa haraka iwezekanavyo baada ya wabunge kupiga kura Juni 30 kuwapa nafasi mashoga kufikia 94,000 Ujerumani kuhalalisha ndoa zao.

Lakini ndoa hizo hazitasajiliwa mpaka mwaka ujao kutokana na kuwa mfumo wa usajili Ujerumani wa kikiritimba hautambui ndoa za jinsia moja.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.