Nahofia jamaa kususia harusi kwa misingi ya kidini

Taifa Leo - - FUMBO & FALAKI -

Shikamoo shangazi. Nina umri wa miaka 25 na nimepata mchumba wa kuoa. Sasa ninajiandaa kufanya harusi kwa misingi ya dini ya Kislamu kwa kuwa mimi ni Muislamu. Hata hivyo, watu wengine wote wa familia yangu ni Wakristo na nahofia huenda wakasusia harusi yangu. Nifanyeje? Kupitia SMS

Hujaelezea iwapo jamaa zako wanaunga mkono au kupinga harusi hiyo. Kama wanakuunga mkono, waalike kwa sherehe kwani harusi ni harusi, iwe ya Kikristo au ya Kislamu. Kama hawataki, itabidi uendelee tu kwani huwezi kuisimamisha sherehe hiyo kwa sababu yao.

Ninamuachia mke pesa lakini nikirudi anataka nijipikie!

Vipi shangazi? Nina mke na sasa ana mimba. Nimekuwa nikimuachia pesa za mahitaji ya nyumbani kila siku nikienda kazini lakini nikirudi ninapata hajapika. Nikimuuliza huchafuka roho bure tu n kuniambia nijipikie. Simuelewi kabisa, nishauri. Kupitia SMS

Kuna uwezekano mkubwa kwamba tabia yake hiyo imetokana na hali yake ya ujauzito na ushauri wangu ni kuwa ujaribu uwezavyo kumvumilia hadi ajifungue ili uone kama mambo yatabadilika.

Nimfanyeje mwenye kumpa mimba binti?

Mimi ni baba ya watoto watano na nahitaji ushauri wako. Kuna mwanamume ambaye amempachika mimba binti yangu mwanafunzi wa Kidato cha Tatu. Tulijua kuhusu mimba hiyo ya miezi sita majuzi tu. Mwenye mimba namjua na sijui nitamfana nini. Nishauri.

Kupitia SMS Kama binti yako hajahitimu umri wa mtu mzima, yaani miaka 18, ni makosa kisheria kwa mwanamume yeyote kushiriki naye mapenzi. Iwapo unahisi hamuwezi kushauriana na kufikia maelewano na mwanamume huyo, una haki ya kumshtaki ili achukuliwe hatua.

Namtafuta mume tulee watoto wangu

Kwako shangazi. Nina umri wa miaka 36 na nina watoto watatu. Natafuta mwanaume mwaminifu anayetaka kuoa na ambaye yuko tayari kunikubali pamoja na watoto wangu. Ninaamini unaweza kutumia ukumbi wako huu kunisaidia. Kupitia SMS

Ninaamini ujumbe wako huu utawafikia wanaume wengi wasomaji wa safu hii na watakaovutiwa watawasiliana nawe. Haitawezekana mimi kukusaidia kwa wewe mwenyewe ndiye unajua aina ya mwanaume unayemtaka kuwa mume wako. Isitoshe, mimi ninapokea tu jumbe za wanaotaka ushauri na siwafahamu.

Nina mume na pia kijana wa pembeni

Hujambo shangazi? Mimi nina mume na tunapendana. Hata hivyo, kuna kijana ambaye nimempenda naye pia ananipenda. Nitamuepuka vipi?

Kupitia SMS

Sielewi unatafuta mapenzi gani zaidi ilhali unasema umeolewa na wewe na mume wako mnapendana. Iwapo hiyo ni kweli, hisia zako kwa kijana huyo zinaongozwa na tamaa tu wala si mapenzi. Isitoshe, mapenzi nje ya ndoa ni haramu. Tulia kwa mume wako na uheshimu ndoa yenu.

Mke amtesa mtoto sababu si wake

Hujambo shangazi? Tafadhali nahitaji ushauri wako. Mke wangu ambaye ni mama wa kambo wa kijana wangu anamtesa sana mtoto huyo hata nikiwepo na nikilalamika anatishia kuniacha. Anampendelea zaidi mtoto tuliyezaa naye.

Ninaamini ulimuoa mwanamke huyo kwa kumpenda na kama naye anakupenda antarajiwa pia kumpenda mwanao. Mtoto wako ni damu yako na kwake kumtesa ni sawa tu na kukutesa wewe. Ni heri muachane kuliko kuendelea kuona mtoto wako akiteswa na mtu anayedai kuwa mke wako.

Alidai ananipenda, sasa nina mimba ameanza kunihepa

Shikamoo shangazi? Nina umri wa miaka 19 na kijana mpenzi wangu amenipa mimba. Sasa ameanza kunihepa akidai si yake. Naomba ushauri wako.

sh10.

Kupitia SMS

Kupitia SMS

Haya ndiyo masaibu yanayowapata vijana wanaoshiriki kiholela mahusiano ya kimapenzi. Bila shaka kijana huyo anakuhepa kwa sababu hataki kuwajibika kulea mtoto na hata akishurutishwa akubali hatakufaa kwa sababu hataki. Jitayarishe kulea mtoto wako wala usimtegemee.

Kama unalo swali lolote unalohitaji ushauri, tuma kwa kwa nambari ya simu ya 21603 ukianza na neno shangazi. Kila ujumbe unagharimu

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.