Nyota

Na Sheikh Khabib

Taifa Leo - - FUMBO & FALAKI -

KONDOO Machi 21 – Aprili 20: Mambo mengi uliyopanga yatafaulu lakini unashauriwa uwekeze kwa mpango. Usiingize pesa nyingi kwenye miradfi ambayo huna hakika nayo kwani kuna hatari ya matapeli kukunyemelea. NG’OMBE Aprili 21 – Mei 20: Umechoka kiasi na naona matembezi ya hapa na pale yatakuletea utulivu wa moyo hata kama ni kuwajulia hali jamaa au marafiki. Hata hivyo, usijaribu kujiingiza katika starehe nyingi ambazo hujapangia. MAPACHA Mei 21 – Juni 21: Rafiki yako wa dhati ambaye hamjakutana kwa muda mrefu anaonekana kuhitaji msaada wako. Tafadhali usimpuuze kwani wewe tu ndiye tegemeo lake. Leo ukimfaa, kesho atakufaa pakubwa zaidi, chukua hatua. KAA Juni 22 – Julai 22: Huenda watu wakakupuuza kwa wakati huu kwani umeishiwa na hawaamini wakikukopesha utawalipa. Usijali. Wanaokudharau leo watakuheshimu na hata kukuhitaji kesho. SIMBA

Julai 23 – Agosti 22: Umekuwa na bidii katika kila jambo unalofanya. Hata hivyo, jasho la bidii yako limekuwa likipotelea usikojua. Si makosa yako, lakini sasa huna budi kuchukua hatua mara moja kurekebisha hali hiyo. Ukichelewa utajuta mwenyewe. MASHUKE Agosti 23 – Septemba 23: Kuna jambo linalokusumbua kuhusiana na kitu kichopotea, kesi, ndoa au mtihani. Usiwe na hofu kwa sababu naona hali yako haitakuwa mbaya hatimaye.

MIZANI Septemba 24 – Oktoba 23: Ikiwa kuna siku ambayo umewahi kupata mabadiliko ya maisha, si nyinine ni hii. Naona itakuwa siku nzuri kwako na mambo yatakwendea vizuri tu. Ili unufaike kikamilifu, una jukumu la kutolegeza juhudi zako katika lolote utakalofanya.

NGE Oktoba 24 – Novemba 22: Inahangaika bure. Wakati huu watu wanaonekana kuwa tayari kukusaidia kusuluhisha matatizo yako. Tumia nafasi hiyo vizuri kwani huja kwa nadra sana katika maisha ya binadamu. MSHALE Novemba 23 – Desemba 21: Utapokea ujumbehata kupigiwakwa ama simu barua-pepe,na mtu Fulani. arafa La au kusikitisha ujumbeni kuwa mzuri hautakuwa bali wa mkosi tu. MBUZI Desemba 22 – Januari 20: Umekuwa ukifa kikondoo kwa muda mrefu, kila mara ukiadhibiwa kwa sababu ya makosa ambayo kamwe hukutenda. Hali yako ya kuvumilia mambo bila kulalamika ndiyo itakayokuangusha maishani.

NDOO Januari 21 – Februari 19: Watu fulani mnaofahamiana vyema watakufuata wakitaka mshirikiane kibishara lakini unashauriwa usikimbilie jambo hilo. Mara nyingi wanaokutapeli huwa watu wa karibu kifamilia au hata marafiki wa muda mrefu. SAMAKI Februari 20 – Machi 20: Unashangaa kwamba baadhi ya marafiki zako wameanza kujitenga nawe na huelewi ni kwa nini. Sababu hasa ni hasira zako za kila mara na itabidi ujirekebishe. Ukitaka uaminifu kutoka kwa wenzako, komesha hasira.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.