Kawangwarekuendelezamavamizi

Taifa Leo - - SPOTI - Na JOHN ASHIHUNDU

MECHI saba za kuwania ubingwa wa Sportpesa Super 8 PL zimepangwa kuchezwa leo na kesho katika viwanja mbali mbali vya Nairobi na vitongoji vyake.

Kesho, Kawangware United ambao wanaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 53 watakuwa ugenini kukabiliana na MASA ugani Makongeni wakati NYSA wanaoshikilia nafasi ya pili kwa pointi 48 wakiwakaribisha Ole Rongai katika uwanja wa Ngong Posta.

Jericho FC walio na pointi 47 katika nafasi ya tatu watakuwa ugenini kuvaana na Kiambiu Youth.

Huku ligi ya timu 16 ikielekea ukingoni, timu tatu zinakabiliwa na hatari ya kushushwa ambazo ni Macmillan FC (23), Kiambiu Youth FC (18) na Ajax Youth (9) wakati Ole Rongai FC (19) wakitegemea mechi zilizobakia.

Katika mechi ya leo Jumamosi, mabingwa watetezi, Kayole Asubuhi watafunga safari hadi Kawangware BP kupepetana na Meltah Kabiria kuanzia saa tisa alasiri.

Asubuhi wanakamati nafasi ya nne kutokana na ushindi mara 42 sare sita ambapo ushindi katika mechi ya leo utawaongezea vijana hao wa kocha Isaiah Omondi nafasi ya kumaliza miongoni mwa nne bora.

Kwenye mechi zao za karibuni, Meltah ambao wamo katika nafasi ya nane wamekuwa wakipata matokeo mazuri dhidi ya timu kubwa zikiwemo Kawangware na Zamalek.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.