Starletsu-2o katikamechi yakufakupona

Taifa Leo - - SPOTI - Na JOHN ASHIHUNDU

TIMU ya taifa ya wanasoka wasiozidi umri wa miaka 20 leo alasiri itajitosa uwanjani kupambana na Ethiopia katika mechi ya wanawake ya mkondo wa pili ya kuwania kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2018. Mechi hiyo itachezewa Kenyatta Stadium mjini Machakos kuanzia saa tisa alasiri.

Timu hizo zilitoka sare 2-2 katika mechi ya mkondo wa kwanza Hawassa Stadium nchini Ethiopia, hivyo wenyeji wanahitaji sare ya aina yoyote kusonga kufuzu kwa hatua ya pili. Washindi katika mechi ya leo atakutana na mshindi kati ya Algeria na Ghana.

Kikosi cha Kenya cha wanasoka 18 kimekuwa kikijiandalia katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani chini ya wakufunzi Caroline Achieng, Ann Aluoch, Jackline Akoth na Musa Otieno.

“Tumejiandaa vya kutosha kwa mechi hii. Tulihangaisha vilivyo katika mechi ya mkondo wa kwanza lakini tukafanikiwa kupata sare,” Otieno alisema jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.