Timu za voliboli zakatiwa umeme na maji Kasarani

Taifa Leo - - SPOTI - Na JOHN KIMWERE

TIMU za taifa za voliboli zimejipata kwenye wakati mgumu baada ya kampuni ya umeme nchini (KPLC) kukatiza huduma hiyo na kudai wasimamizi wa uwanja wa Kasarani hawajalipia ada hiyo kwa muda mrefu.

Jana kwa siku ya nne mfululizo timu za voliboli (wanaume na wanawake) pia ile ya soka ya Nairobi Water zilikosa kuendeleza ratiba yake ipasavyo kwa kukosa huduma za umeme.

Ukosefu wa umeme umechangia pia kutokuwapo kwa maji, afisa wa kamati ya kiufundi wa KVF, David Lung’aho alisema. “Tuna wakati mgumu maana muda umeyoyoma. Timu ya wanawake inajiandaa kushiriki fainali za kombe la Afrika (CAVB) nchini Cameroon kuanzia wiki ijao.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.