Kenya yaaga michezo kwa kulemewa

Taifa Leo - - Front Page - Na GEOFFREY ANENE

KENYA imebaki na maswali mengi kuhusu jinsi ilivyokosea baada ya kuandikisha matokeo mabaya kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 katika makala ya 21 yaliyokamilika nchini Australia, jana.

Mabingwa hawa wa riadha duniani mwaka 2015 walikamilisha ziara ya mji wa Gold Coast katika nafasi ya 14 kutoka orodha ya timu 71 kwa medali 17 (dhahabu nne, fedha saba na shaba sita). Siku ya mwisho ilikuwa ya masikitiko makubwa kwa sababu Kenya iliambulia pakavu katika mbio za kilomita 42 licha ya kupigiwa upatu kupata medali.

Kabla ya kufunga safari ya kuelekea Gold Coast, kambi ya Kenya ilijawa matumaini na hata kujipiga kifua itaimarisha idadi ya medali zake kutoka 25 (dhahabu 10, fedha 10 na shaba tano) ilizopata miaka minne iliyopita mjini Glasgow, Scotland.

Hata hivyo, dalili za Kenya kufanya vibaya zilianza kuonekana pale mabondia Nicholas Okoth, Elly Ocholla, Edwin Owuor, Benson Gicharu na Lorna Simbi walipobanduliwa nje mapema.

MANCHESTER City walinusia zaidi taji la tano la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) baada ya kujinyanyua ugenini na kuwapokeza Tottenham Hotspur kichapo cha mabao 3-1 uwanjani Wembley mwishoni mwa wiki jana.

Kushindwa kwa Tottenham kuliwapa Chelsea matumaini finyu ya kutinga mduara wa nnebora na hivyo kufuzu kwa kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao baada ya kutoka nyuma na kuwakomoa Southampton 3-2 ugani St Mary’s.

Kwa upande wao, Liverpool waliimarisha zaidi nafasi yao ya kukamilisha kampeni za msimu miongoni mwa nne-bora kwa kuwachabanga Bournemouth 3-0 katika mchuano uliompa nyota Mohamed Salah jukwaa mwafaka kufunga bao lake la 40 akiwasakatia waajiri wake katika mapambano yote.

Man-city walipoteza nafasi ya kutia kapuni ubingwa wa EPL msimu huu mbele ya mashabiki wao wa nyumbani yapata wiki moja iliyopita baada ya utepetevu wao kuwaruhusu Manchester United kutoka nyuma na kuwapokeza kichapo cha 3-2.

Masaibu ya mabingwa hao watarajiwa wa soka ya Uingereza yalizidishwa na Liverpool wiki jana baada ya kubanduliwa kwenye robo-fainali za UEFA kwa jumla ya mabao 5-1.

Ingawa hivyo, Pep Guardiola aliwachochea vijana wake kudhihirisha ukubwa wa uwezo walionao uwanjani kwa kuyazima kirahisi makali ya Tottenham ambao chini ya kocha Mauricio Pochettino, ilikuwa mara yao ya kwanza kuzidiwa maarifa ligini tangu walipolizwa na Man-city ugani Etihad mnamo Desemba 2017.

Nyota Gabriel Jesus aliwafungulia Man-city ukurasa wa mabao kunako dakika ya 22 kabla ya Ilkay Gundogan kuongeza la pili kupitia mkwaju wa penalti dakika tatu baadaye na hivyo kuyumbisha kabisa chombo cha Tottenham ambao kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne kwa alama 67, saba zaidi kuliko Chelsea wanaoshikilia nafasi ya tano.

Bao la tatu la Man-city lilifumwa wavuni na winga Raheem Sterling aliyechangia pia kupatikana kwa penalti iliyofungwa na Gundogan ila marejeleo ya picha za video yalionesha baadaye kwamba Sterlinga alikabiliwa visivyo na kipa Hugo Lloris nje ya msambamba wa Tottenham.

Liverpool wanafunga mduara wa nne-bora kwa alama 70 japo pengo la pointi 17 linatamalaki kati yao na Man-city ambao hadi Man-united waliposhuka dimbani kuvaana na West Bromwich Albion uwanjani OID Trafford hapo jana, walikuwa wakiwazidi kwa alama 16.

Sawa na jinsi ilivyokuwa katika mchuano uliowakutanisha Man-city na Man-united, vijana wa Guardiola nusura wawaruhusu Tottenham pia kurejea mchezoni katika kipindi cha pili baada ya nyota Christian Eriksen kumpiku beki Aymeric Laporte na kufunga.

Picha/ AFP

Wanariadha washiriki marathon katika Michezo ya Jumuiya ya Madola jijini Gold Coast, Australia, jana. Kenya haikushinda medali yoyote katika mbio hizo.

Picha/afp

Kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne (kushoto) ampiku kiungo wa Tottenham Hotspur, Dele Alli katika mechi ya ligi kuu uwanjani Wembley, Jumamosi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.