Onyo kwa wanaouza dawa katika hospitali za umma

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na BRIAN OCHARO

SERIKALI ya Kaunti ya Taita Taveta imenunua dawa za thamani ya zaidi ya Sh39.5 milioni kuboresha huduma za afya.

Akiongea katika hafla ya kugawa hizo dawa, Waziri wa Afya katika kaunti hiyo Dkt Frank Mwangemi ametoa onyo kwa wauguzi wa afya kuwa watachukuliwa hatua ya kisheria wakipatikana wakiziuza.

Alisema serikali ya kaunti inapeleleza madai ya ulaghai kuhusu uuzaji dawa.

“Gavana ameongea na EACC kusaidia kujua jinsi dawa zimekuwa zikipotea kwenye vituo vyetu vya afya. Wahusika wakijulikana watakabiliwa kisheria,” alisema Bw Mwangemi.

Waziri huyo alisema wauguzi wa afya ambao huenda wakapatikana na kosa la kuuza dawa za umma watafutwa kazi na hatua pia washtakiwe.

Wakiongozwa na Kiongozi wa wengi katika bunge la Kaunti, Bw Jason Tuja, viongozi wa kaunti waliapa kudhibiti visa hivyo, ambavyo kwa muda vimekuwa vikishuhudiwa.

Bw Tuja amesema ni sharti kwa huduma zinazotolewa kwa hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kufikia kiwango cha kitaifa.

Picha/maktaba

Muuguzi akihudumia mgonjwa katika Hospitali ya Kaunti ya Siaya majuzi. Serikali ya kaunti ya Taveta imeonya wauguzi na watu wengineo watakaopatikana wakiuza dawa za hospitali za umma eneo hilo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.