Jubilee na NASA wazidi kupongeza muafaka wa Raila, Uhuru

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na SHABAN MAKOKHA

WANASIASA kutoka mirengo ya Jubilee na Nasa mnamo wikendi waliendelea kusifia mwafaka wa makubaliano kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.

Aidha, walisema kwamba mwafaka huo ni muhimu sana katika kuleta umoja wa kitaifa.

Viongozi hao walikutana wakati wa hafla ya makaribisho ya Waziri wa Elimu Amina Mohames katika Kaunti ya Kakamega.

Viongozi wa Jubilee, wakiongozwa na mbunge Bernard Shinali (Ikolomani) walisema kwamba wangali wanawafikia wenzao katika Nasa, kuondoa tofauti zao za kisiasa ili kustawisha maendeleo.

“Wakati wa siasa umeisha, hasa baada ya Rais Kenyatta na Bw Odinga kusalimiana. Kwa sasa tunapaswa kuangazia njia za kuwahudumia Wakenya ili kuimarisha uchumi wetu,” akasema Bw Shinali.

Wengine waliokuwepo ni mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria, Johnson Naicca (Mumias Magharibi), Seneta wa Kakamega Cleophas Malala kati ya wengine.

Naibu Rais William Ruto alisema wakati umefika viongozi kuanza kuwahudumia wananchi.

Gavana Wycliffe Oparanya alisalimiana na Bi Mable Mururi, aliyekuwa mpinzani wake mkuu katika kinyang’anyiro cha ugavana. Bi Muruli aliahidi kushirikiana na Bw Oparanya katika kuiendeleza kaunti hiyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.