France, Spian mataifa ghali zaid fainalini

Taifa Leo - - Front Page - Na CHRIS ADUNGO

JOSEPH Phillip Yobo, 37, ni kiungo wa zamani wa Nigeria ambaye hadi kustaafu kwake katika ulingo wa soka ya kimataifa mnamo Juni 2014, alikuwa nahodha wa

Super Eagles. Hadi kufikia sasa, Yobo anayemiliki akademia kubwa za soko mijini Ogoni na Lagos, ndiye mshikilizi wa rekodi ya mchezaji ambaye amecheza mara nyingi zaidi (101) na timu ya taifa ya Nigeria.

Maarifa na ubunifu wa Yobo ulitegemewa sana na Nigeria katika fainali tatu zilizopita za Kombe la Dunia na sita za kuwania ubingwa wa Kombe la Afrika (AFCON).

Akiwa mzawa wa mtaa wa Kono viungani mwa mji wa Khana River States, Yobo aligundua kipaji chake katika soka akiwajibikia kikosi cha Michellin-harcourt, Nigeria kati ya 1996 na 1997.

Mnamo 1998, Yobo aliagana rasmi na Michellin-harcourt na kutua nchini Ubelgiji kuvalia jezi za Standard Liege. Baada ya kuaminiwa kusakata mchuano wake wa kwanza kambini mwa Standard Liege mnamo 2000, Yobo kiwango cha kurudhisha kwake uwanjani k ilimpa uhakika wak u unga kikosi cha kwanza cha klabu hiyo iliyomwajibisha mara 46 hadi kufikia mwisho wa 2001.

Mabao mawili muhimu aliyowafungia waajiri wake mwishoni mwa 2000-01 yaliwachochea Olympique Marseille kumtaka kiungo huyo. Baada ya majeraha kuyalemaza pakubwa makali yake mnamo 2001, Yobo alitumwa kwa mkopo kuvalia jezi za Tenerife katika visiwa vya Canary, Uhispania. Alikihudumia kikosi hicho kwa jumla ya miezi tisa kabla ya kurejea Marseille kisha kujiunga na Everton kwa mkopo mwingine wa mwaka mmoja mnamo Julai 2002. Iliwalazimu Everton kuweka mezani kima cha Sh150 milioni ili kumtia Yobo katika sajili rasmi ya kikosi hicho chini ya kocha David Moyed. Kuimarika kwa makali yake ugani Goodison Park kulimwek a Moyes katika ulazima wa kumpokeza Yobo mkataba wa kudumu mwishoni mwa 2003. Usajili wake ulirasimishwa kwa kima cha Sh600 milioni.

Yobo alijipa uhakika wa kukamilisha kikosi cha kwanza cha Everton kiasi kwamba alikuwa sehemu ya wachezaji saba waliowajibishwa katika kila dakika ya kila mchuano katika msimu mzima wa 200607. Mwingine aliyeunga kikosi hicho ni aliyekuwa beki mahiri wa timu ya taifa ya Uingereza, Joleon Lescott, 35.

Kukawia kwa Yobo kurefusha muda wa kuhudumu kwake ugani Goodison Park mnamo 2006 kulimweka nyota huyo katika ulazima wa kuhusishwa pakubwa na Arsenal. Hata hivyo mnamo Julai 22, alitia kidole kwenye mkataba mpya uliopania kumdumisha kambini mwa Everton hadi mwishoni mwa 2010.

Mnamo Aprili 15, 2007, Yobo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji asiyekuwa mzawa wa Uingereza kuchezea Everton idadi kubwa zaidi ya michuano. Aliishikilia rekodi hiyo hadi mapema 2012.

Jeraha lililomweka mkekani nyota Phil Neville mnamo Oktoba 2007 liliwachochea vinara wa benchi la kiufundi la Everton kumpokeza Yobo utepe wa unahodha katika mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) uliowakutanisha na Larissa ya Ugiriki.

Kwa hatua hiyo, Yobo aliingia katika mabuku ya historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza mzawa wa Afrika kuwahi kushikilia mikoba ya unahodha kambini mwa Everton.

Mnamo Mei 6, 2009, Yobo aliwafungia Everton bao lake la kwanza la msimu dhidi ya West Ham na hivyo kuwachochea kujivunia ushindi muhimu wa 3-1 katika mchuano huo wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Katika kampeni nzima za msimu wa 2009-10, ilimjuzu Yobo kusuka mfumo mpya uliooana na wa beki Sylvain Distin baada ya Lescott na Phil Jagielka waliotegemewa sana katika safu ya nyuma ya Everton kupata majeraha yaliyowaweka nje ya kikosi hicho kwa kipindi kirefu.

Mnamo Novemba 29, 2009, Yobo alijifunga katika mechi iliyowashuhudia Everton wakititigwa na Liverpool mabao 2-0 kwenye gozi la Merseyside ugani Anfield. Kupona kwa Distin, Jagielka na John Heitinga ni tukio lililomweka Yobo katika ulazima wa kusugua benchi katika michuano yote iliyosalia katika msimu wa 2009-10.

Mnamo Agosti 31, 2010, Yobo alitia saini mkataba wa mwaka mmoja na Fenerbahce ya Uturuki.

Aliwajibishwa katika jumla ya michuano 30 na akafunga bao moja. Ukubwa wa ushawishi wake ulikuwa kiini cha Fenerbahce kutia kapuni ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki mwishoni mwa msimu wa 2010-11.

Mnamo Septemba 6, 2011, Fenerbahce na Everton walifikia makubaliano mapya kuhusu mkataba mwingine wa mkopo wa mwaka mmoja uliomshuhudia Yobo akidumishwa nchini Uturuki, ila mara hii kwa mkataba wa miaka mitatu. Hatua hiyo ilikatiza rasmi uhusiano wa miaka 10 aliokuwa nao na Everton.

Bao lake la kwanza kambini mwa waajiri wake hao lilikuwa mnamo Agosti 17 dhidi ya Torku Konyaspor. Baada ya kandarasi yake na Fenerbahce kutamatika rasmi mnamo Agosti 31, 2013, Yobo alisajiliwa na Norwich City mwishoni mwa Januari 2014. Mchuano wake wa kwanza ndani ya jezi za kikosi hicho ni kibarua kilichowakutanisha na Manchester City mnamoi Februari 2014.

Mnamo 2010, Yobo alifunga pingu za maisha na mwigizaji Adaeze Igwe, miezi mitatu pekee baada ya kuanza kutoka pamoja kimapenzi mwishoni mwa Desemba 2009. Kwa pamoja, wamejaliwa mtoto mmoja wa kiume, Joey aliyezaliwa mnamo Aprili 2010.

Yobo ana kaka wawili - Albert na Noruma ambao kwa pamoja waliwahi kupiga soka kambini mwa Super Eagles ya Nigeria hadi walipostaafu rasmi mwishoni mwa Julai 2008.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.