Uhuru kueleka Uingereza kwa mkutano

Taifa Leo - - News - Na LEONARD ONYANGO

RAIS Uhuru Kenyatta leo anatarajiwa kuelekea nchini Uingereza ambapo atahudhuria kongamano la wakuu wa serikali kutoka mataifa 53 ambayo ni wanachama wa Jumuiya ya Modala jijini London.

Kulingana na Msemaji wa Ikulu Monoah Esipisu, Rais Kenyatta katika ziara yake ya siku tano, atakutana na Malikia wa Uingereza Elizabeth II na Waziri Mkuu wa Theresa May kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara.

“Ziara ya Rais Kenyatta inatarajiwa kuboresha ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na usalama baina ya Kenya na Uingereza. Rais pia atakutana na wakuu

wa serikali mbalimbali na wawekezaji ambapo atajadili suala la kuboresha utalii na masuala mengineyo ya kiuchumi,” akasema Bw Esipisu alipokuwa akihutubia wanahabari jana katika Ikulu ya Nairobi.

Alisema Rais pia atakutana na wawekezaji Wakenya wanaoishi nchini Uingereza. Uingereza ni moja ya masoko makuu ya chai na maua yanayokuzwa humu nchini.

“Rais Kenyatta atahuhutubia kongamano la wawekezaji nchini Uingereza na ataelezea hatua ambazo zimepigwa na Kenya katika ukuzaji wa uchumi na udumishaji wa amani kwenye ukanda wa Afrika Mashariki,” akasema Bw Esipisu.

Kesho, Rais Kenyatta atazuru Soko la Hisa la London ambapo atakutana na wawekezaji nchini Uingereza kujadili masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Kilele cha kongamano hilo kitakuwa Ijumaa ambapo viongozi wa serikali watahudhuria maakuli katika eneo la Windsor Castle.

Picha/maktaba

Rais Kenyatta (pili kulia) katika safari ya awali.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.