KNEC yatoa masharti makali ya mitihani

Taifa Leo - - News - Na Ouma Wanzala

BARAZA la Kitaifa la Mitihani (KNEC) limeanzisha kanuni kali za usalama katika usimamizi wa mitihani, ambazo zitazuia utoaji nakala za mitihani hiyo.

Hili linalenga kukabili wizi wa mitihani, ambao umekuwa tatizo kuu.

Ina maana kuwa wanafunzi ambao hawatatathmini upya maelezo yao hawataruhusiwa kuufanya mtihani Novemba, ikiwa kutakuwa na matatizo yoyote kuhusu maelezo yao.

Zoezi hilo litaanza leo na kumalizika mnamo Ijumaa. Jumla ya wanafunzi 1, 060, 787 wamesajiliwa kufanya mtihani huo. Kulingana na KNEC, wakuu wa shule ambako makosa hayo yatapatikana wataadhibiwa na Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC).

“Kutokana na tishio za usalama ambazo husababishwa na utoaji nakala wa karatasi za mitihani, KNEC imejitolea kuhakikisha kwamba vifaa vya kuendeshea mtihani huo vimewekewa usalama wa kutosha,” akasema Afisa Mkuu Mtendaji wa baraza hilo Bi Mercy Karogo kwenye notisi aliyotuma kwa wakuu wa taasisi mbalimbali za elimu.

Notisi hiyo pia ilitiwa saini na Afisa Mkuu Mtendaji wa TSC Bi Nancy Macharia.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.