Wahadhiri walio katika mgomo waomba kuonana na Rais

Wakuu wa UASU na KUSU wasema ni Uhuru pekee anayeweza kutatua mzozo

Taifa Leo - - Front Page - NAIROBI Na CECIL ODONGO Ili kutolea maoni habari hii, nenda kwa taifaleo.nation.co.ke

MUUNGANO wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU) na Chama cha Wafanyakazi wa Vyuo Vikuu (KUSU) sasa wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta aingilie kati na akutane nao ili kutafuta njia za kumaliza mgomo wao ambao umelemaza shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini

Katika kikao na wanahabri katika jumba la Unafric jana, viongozi hao walisisitiza kwamba ni Rais Kenyatta pekee watakayemsikiza na kutaja kuendelea kushiriki majadiliano na wizara ya Elimu kama kupoteza wakati.

Katibu Mkuu wa UASU Constantine Wasonga amesema kwamba pendekezo lililowasilishwa na wizara hiyo lilikuwa la mzaha na kejeli kwa jitihada zao za kutaka muafaka wao wa 2017-2022 ujadiliwe na utekelezwe.

“Sisi tunapigania mshahara mzuri si suala la likizo wala umri wa kustaafu. Tukilipwa vizuri hata tukistaafu mapema hatuna shida,” akasema Wasonga.

Katibu huyo alisisitiza kwamba Kamati ya Bunge kuhusu elimu ilielekeza hazina ya fedha kuwasilisha pendekezo faafu litakalowiana na muafaka wao lakini hilo halijaangaziwa kwenye pendekezo walilopokea.

“Wakati wabunge walielekeza Baraza la usimamizi wa vyuo vikuu liwasilishe pendekezo haikuwa na maana tuletewe mambo ambayo hayahusu tunachopigania,” akateta vikali Wasonga.

Aidha, Katibu Mkuu wa KUSU Charles Mukhwana alidai kwamba kuna njama fiche ya kusambaratisha vyuo vikuu vya umma ili vile vya kibinafsi vistawi.

“Iweje kabla hatua yoyote ipigwe katika kuboresha malipo ya wahadhiri lazima mgomo uitishwe. Iwapo muafaka wetu utatimizwa basi tunawahakikishia wanafunzi wetu kwamba masomo haya tasa m bara tishwa kwa kipindi cha miaka minne ijayo,” akasisitiza.

Alilaumu Waziri wa Elimu Amina Mohamed kwa kukimbilia kuandaa hafla ya makaribisho na kufumbia jicho zaidi ya wanafunzi 600,000 ambao hawajafundishwa kwa siku 46 ambazo mgomo wao umedumu.

Picha/maktaba

Katibu Mkuu wa Chama cha Wahadhiri wa Vyuo Vikuu (UASU) Constantine Wasonga (kulia) akimsalimia afisa wa chama katika mkutano wa Machi 18, 2018. Wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu wanataka kuonana na Rais ili kutatua mgomo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.