Mancity watwaa taji la ligi, walenga rekodi ya EPL

Taifa Leo - - Front Page - LONDON, Uungereza

BAADA ya Manchester City kutia kapuni ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo Jumapili, kocha Pep Guardiola amewataka vijana wake kuelekeza macho kwenye mechi zilizosalia kwa lengo la kuweka rekodi zaidi katika historia ya ligi hiyo.

Man-city ambao wametamalaki sana kivumbi cha EPL msimu huu, walitawazwa wafalme wa Uingereza baada ya wapinzani wao wakuu, Manchester United kuduwazwa na West Brom kwa kichapo cha bao 1-0 uwanjani Old Trafford.

Chini ya Guardiola, Man-city wanajivunia pengo la alama 16 kati yao na Man-united ambao wanashikilia nafasi ya pili kwa sasa na wana uwezo wa kujizolea jumla ya pointi 15 pekee kutokana na michuano mitano iliyosalia

ligini muhula huu.

Man-city wataandaliwa gwaride la heshima mbele ya mashabiki wao wa nyumbani mwishoni mwa wiki hii katika mechi itakayowakutanisha na Swansea City ugani Etihad.

Ingawa hivyo, Guardiola amewataka vijana wake kumaliza kampeni za msimu huu kwa matao ya juu, kwa kusajili ushindi mnono utakaoendeleza ubabe wao katika michuano mitano iliyosalia.

Wakitegemea makali na ubunifu wa nyota Kevin De Bruyne, David Silva, Sergio Aguero na Raheem Sterling, Man-city waliweka rekodi mpya katika EPL mapema msimu huu kwa kushinda jumla ya mechi 18 mfululizo ligini.

Guardiola amewahimiza vijana wake kuivunja rekodi ya Chelsea waliofanikiwa kujizolea jumla ya pointi 95 katika EPL mnamo 2004-05.

Hiyo ni rekodi ambayo Man-city wana uwezo wa kufikia na hata kuipiku iwapo watajinyakulia jumla ya alama tisa pekee kutokana na michuano mitano iliyopo mbele yao kwa sasa.

Wakijivunia kusajili ushindi mara 28 katika jumla ya mechi 33 za EPL msimu huu, Man-city wanahitaji kuwabamiza wapinzani waliopo mbele yao mara tatu pekee ili kuvunja rekodi ya Chelsea walioshinda mechi 30 mnamo 2004-05.

Rekodi ya Man-united ambao waliwahi kutia kapuni ubingwa wa EPL baada ya kudumisha pengo la alama 18 kati yao na Chelsea walioshikilia nafasi ya pili mnamo 2000, ipo katika hatari ya kuvunjwa na Man-city msimu huu.

Iwapo Man-city watasajili ushindi katika michuano miwili zaidi ya ugenini msimu huu, basi wataivunja rekodi ya Chelsea ambao waliwapiga wageni wao wa EPL kwenye jumla ya michuano 15 mnamo 2004-05.

Kutokana na jinsi ambavyo Man-city wamekuwa wakimgeuza takriban kila mpinzani kuwa mnyonge machoni pao msimu huu, ilikuwa wazi

la pili mwishoni mwa dakika ya 58.

Bao jingine la PSG lilifumwa wavuni na fowadi Julian Draxler mwishoni mwa kipindi cha pili, Mchoro kwenye uwanja wa Etihad mjini Manchester waonyesha wanasoka wa Manchester City wakisherehekea ushindi wa taji la Ligi Kuu ya Uingereza mnamo Aprili 15, 2018. Picha ndogo: Mbwa avalishwa sare ya Mancity baada ya mashabiki kuanza kusherehekea ubingwa.

kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita kwamba ni lini wala si iwapo, vijana wa G u a r d i o l a wangetawazwa mabingwa wa EPL.

Kwa mujibu wa wadadisi wa soka ya Uingereza, fahari na tija zaidi kwa

Guardiola na kikosi chake ni utamu wa kutawazwa wafalme wa EPL baada ya kujikwaa wa maadui wao Manunited

ambao waliwakomoa zaidi ya wiki moja iliyopita katika gozi la Manchester lililowakutanisha ugani Etihad.

Ufanisi wa kutia kapuni ufalme wa EPL zikiwa zimesalia mechi tano zaidi kwa kipenga cha mwisho katika ligi hiyo kupulizwa rasmi ni jambo lililowafanya Man-city kuifikia rekodi ya Man-united waliofikia mafanikio sawa na hayo katika kampeni za msimu wa 200001.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.