Moi aombe aila ya Matiba msamaha, asema Koigi

Taifa Leo - - Front Page - Na PETER MBURU

MPIGANIAJI wa ukombozi wa pili Koigi Wa Wamwere jana alimtaka rais mstaafu Daniel Moi kuomba familia ya marehemu Kenneth Matiba msamaha, kwa mateso aliyopitia ndani ya uongozi wake, huku wazee wa Bonde la Ufa wakiitaka serikali kumzika kishujaa kama alivyozikwa Nelson Mandela.

Bw Wamwere alisema kuwa kifo cha Bw Matiba kilitokana na shida za kiafya alizopata wakati alipofungwa bila hukumu, na mateso aliyokumbana nayo akiwa jela.

Mbunge huyo wa zamani wa Subukia alimtaka Mzee Moi kuwa jasiri na kuiomba msamaha wakati taifa likiomboleza kifo cha kiongozi huyo, akisema ujumbe wa rambirambi haungetosha.

Alimtaja Bw Matiba kuwa kiongozi aliyejitolea kupigania Kenya huku akiitaka serikali kukiri makosa ya uongozi wa mbeleni mbele ya umma kama namna ya kuonyesha kufurahia matunda aliyopigania marehemu Bw Matiba.

“Ninatarajia kuwa siku zijazo wakati taifa likiomboleza, mzee Moi atapata ujasiri wa kuomba familia ya Matiba msamaha, mbali na kutuma rambirambi kwani ni kutokana na kifungo alichopata wakati wa Moi na mateso yaliyofuata vilivyompa magonjwa ambayo alirudi nyumbani nayo na kufa baadaye,” Bw Wamwere akasema.

Picha/maktaba

Aliyekuwa Mbunge wa Subukia Koigi Wa Wamwere akihutubia wanahabari awali. Amemtaka Rais Mstaafu Moi kuiomba familia ya marehemu Matiba msamaha kuhusiana na mateso aliyopata chini ya utawala wake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.