Mashini 100 za kamari zanaswa katika operesheni kali ya polisi

Taifa Leo - - Buriani Matiba - Na Gerald Bwisa

MAAFISA wa Polisi kutoka Kaunti ya Trans Nzoia walinasa zaidi ya mashine 100 za kamari katika operesheni ya kipekee iliyofanyika katika mji wa Kitale.

Mkuu wa Polisi wa Trans Nzoia Mashariki Jackson Mwenga amesema kwamba wanaomiliki mashine hizo watashtakiwa mahakamani kwa sababu hawakuwa na vibali vinavyowaruhusu kuendesha biashara ya uchezaji kamari.

“Tunataka kumaliza mtindo mbaya wa uraibu wa kucheza kamari ambao umeshamiri mno hapa Kitale. Cha kuhofisha zaidi ni kwamba vituo hivyo ni vingi na havina lesini za kuwaruhusu kuhudumu,” aliambia wanahabari katika ofisi yake.

Aliahidi kwamba operesheni hiyo itaendelea hadi wakomeshe kabisa tabia ya vijana kutofanya kazi za kujiinua na badala yake kuzamia mchezo huo wa bahati nasibu wakitarajia miujiza ya kushinda pesa nyingi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.