Katibu Knut aomba serikali isianze kushika mabasi yasiyopakwa rangi

Taifa Leo - - Buriani Matiba - Na Joseph Wangui

KATIBU Mkuu wa Chama cha Walimu wa Shule za Upili tawi la Kaunti ya Laikipia Ndung’u Wangenye ameiomba serikali isitekeleze amri ya kuyashika mabasi ya shule ambayo bado hayajapakwa rangi ya manjano.

Bw Wangenye ambaye pia ni mshirikishi wa chama hicho katika ukanda wa Mlima Kenya amesema baadhi ya shule hazijapata pesa za kugharamia kazi hiyo na itakuwa bora iwapo makataa ya Tarehe 31 Aprili yasukumwe mbele.

“Shule nyingi hazina pesa na serikali ilionya vikali walimu wakuu dhidi ya kutoza ada ya kupaka rangi mabasi hayo. Serikali inafaa itenge fedha maalum kwa shughuli hiyo ama iwape shule muda zaidi wakisubiri pesa,” akasema.

Kulingana na katibu huyo, gharama ya kupaka basi ni kati ya Sh60,000 hadi 100,000 ambazo ni ghali mno.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.