Mahakama yatupa rufaa kuhusu kuharamisha ushindi wa Sonko

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Richard Munguti

JARIBO la wapinga kura wawili kuharamisha ushindi wa Gavana Mike Sonko Mbuvi lilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa.

Majaji Roselyn Nambuye, Kathurima M’inoti na Stephen Kairu Gatembu walitupilia mbali rufaa iliyowasilishwa mwanaharakati Japheth Muroko na Zacheus Okoth wakisema Jaji Msagha Mbogholi alikosea kuitupilia mbali kesi waliyomshtaki Bw Sonko.

Mabw Muroko na Okoth walikuwa wameomba mahakama ya rufaa iamuru kesi ya kupinga ushindi wa Bw Sonko wa Agosti 8, 2017 ifufuliwe na mlalamishi mwingine baada ya Jaji Msagha Mbogholi kutupilia mbali kesi hiyo Janauri 9, 2018.

Jaji Mbogholi alifutilia mbali kesi dhidi ya Bw Sonko wapiga kura hao walipokosa kufika kortini kutoa ushahidi wakidai maisha yao yalikuwa hatarini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.