Wavuvi na mabaharia wataka bodi mpya ya majanga baharini

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Kalume Kazungu

WANACHAMA wa muungano wa wavuvi na mabaharia katika kaunti ya Lamu, wanataka kuundwe bodi maalum itakayoshughulikia majanga ya baharini eneo hilo.

Waliwaambia wanahabari mjini Lamu jana kwamba kwa sasa hakuna mikakati yoyote ya kueleweka inayoweza kusaidia kukabiliana na athari za ajali za baharini.

Msemaji wa Muungano huo, Bw Musa Faraj, alisema japo kaunti iliahidi kubuni kitengo cha kukabiliana na majanga ya baharini, kufikia sasa hakuna hatua yoyote imechukuliwa.

“Sisi haturidhishwi na kukosekana kwa kitengo au bodi ya kukabiliana na majanga baharini hapa Lamu. Wakazi wa hapa hasa wavuvi tegemeo lao ni bahari. Usafiri wa hapa pia ni wa baharini,” akasema.

Alipendekeza kuanzishwe kitengo cha wapiga-mbizi watakaoshika doria baharini usiku na mchana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.