Serikali yasambaza miche ya kawaha kuinua uchumi

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Oscar Kakai

SERIKALI ya kaunti ya Pokot Magharibi imesambaza miche ya kahawa kwa wakulima wa eneo hilo bila malipo, kama njia kuwainua kiuchumi na kuwafanya waache ufugaji wa kuhamahama na kuanza kulima mazao ya kuuza.

Gavana wa kaunti hiyo, Prof John Lonyangapuo (pichani) ambaye aliongea mjini Kapenguria kwenye uzinduzi wa miche ya kahawa, alisema kuwa mradi huo wa kwanza ambao unagharimu Sh8 milioni unalenga zaidi ya wakulima 500 kila mwaka.

Alisema kuwa wameanzisha miradi ya kuwaletea wakazi mapato kupitia kwa kilimo, ambayo itasaidia kuinua wakulima kupitia kwa mbinu bora za kisasa. Prof Lonyangapuo alisema kuwa hatua hiyo ya kupanda kahawa itasaidia kupunguza umasikini, ujinga kwenye kaunti hiyo sababu wazazi watakuwa na mbinu mbadala za kujikimu na kujipatia riziki.

“Tumebandikwa majina kuwa sisi ni wezi wa mifugo kwa miaka mingi suala ambalo linazuia uchumi wa watu wetu kuimarika. Kaunti yetu inataka kuwacha kutegemea kufuga mifugo pekee bali kutegemea kilimo cha mazao,” akasema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.