Ugaidi: Washukiwa 5 wakana kupanga mashambulio jijini

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Richard Munguti

WASHUKIWA watano ugaidi waliokuwa wameorodhesha majengo ya Serikali ya kushambulia miongoni mwayo Mahakama kuu ya Milimani walishtakiwa jana mbele ya hakimu mkuu Bw Francis Andayi.

Mabw Abdimajit Adan, Mohammed Osman Nane, John Maina Kiarir , Antony Kitila Makau almaarufu Rasta na Bi Lydia Nyawira Mburu walikanusha mashtaka tisa ya kufanya njama za kutekeleza mashambulizi ya kigaidi mnamo Februari 15 mwaka huu.

Kiongozi wa mashtaka Bw Solomon Naulikha alimweleza Bw Andayi kwamba maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi waliwatia washtakiwa nguvuni kufuatia habari za kijasusi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.