Mzee akwama hospitalini India kwa deni la Sh5m

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Magati Obebo

MZEE mmoja katika eneo la Nyaramba, Kaunti ya Nyamira amekwama katika hospitali moja nchini India kwa kushindwa kulipa deni la Sh5 milioni.

Msemaji wa familia ya mwathiriwa Bw Dickson Nyanyuki alisema kwamba, babake Ezekiel Atoni alipelekwa kupata matibabu maalum katika Hospitali ya Apollo Navi nchini India, ila hajaweza kuondoka kufikia sasa.

Alienda kupokea matibabu ya maumivu ya kichwa.

Alisema kwamba Bw Atoni amekuwa akiugua ugonjwa huo tangu mwaka 2007.

Alisema kwamba babake anahitaji kufanyiwa upasuaji zaidi, hali ambayo imeongeza kiwango cha fedha zinazohitajika.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.