Wakimbizi 5 watozwa faini ya Sh2,000 kwa kuishi wasikostahili

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Oscar Kakai

WAKIMBIZI watano wamehukumumiwa katika mahakama ya Kapenguria kwa kuishi eneo ambalo hawastahili bila idhini.

Aziza Mohammed, Haluwo Abdi, Mirriam Abdi, Ayub Mohammed na Shanifo Hassan, walikamatwa wiki jana na polisi wa Makutani kwenye kizuizi cha barabara kuu ya Kapenguria - Kitale.

Hakimu mwandamizi wa mahakama ya Kapenguria, Bw Vincent Adeti aliwatoza faini ya Sh2,000 kila mmoja au wafungwe siku 30 gerezani.

Walilipa faini hiyo huku hakimu akiamuru warejeshwe kambini Kakuma.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.