Kero la nungunungu kwa wakulima

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na PETER MBURU

MAMIA ya wakulima kutoka eneo la Rongai, Nakuru wanapata hasara kutokana na nungunungu wanaovamia mimea yao.

Hii ni licha ya mavamizi makali kutokana na wadudu waharibifu wa viwavi jeshi.

Wakulima hao sasa wamelazimika kuwekeza katika nyua za waya katika mashamba yao, ili kuzuia wanyama hao kuingia mashambani, baada ya mbinu za mbeleni kugonga mwamba.

Kulingana na wakazi wa eneo hilo, wanapovamia mashamba yao wanyama hao hula takriban kila aina ya mmea, wakivamia mizizi, matawi na hata matunda .

“Wanaopoingia shambani wanakula kila aina ya mmea, kuanzia ndizi, mihogo, viazi, viazi vitamu na hata mahindi na wanakula mizizi, matunda ya vyakula na kuharibu mmea kabisa,” akasema Bi Priscuilla Thumbi, mkulima.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.