Wanyima yaya kibarua eti ahatarisha ndoa zao

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale - Na Richard Maosi

WANAWAKE wa mtaa huu walimpiga marufuku mwanadada mmoja kufanya kazi katika nyumba zao wakidai ana tabia ya kupumbaza na kutekenya hisia za mapenzi za waume wao.

Penyenye zinaarifu mwanadada alitegemea kazi za yaya mchana katika nyumba za wadosi lakini akawa akiteka wanaume na kuwa tisho kwa ndoa. ‘’Licha ya wanaume kumpigia debe kama mchapa kazi, uwepo wake ulizidi kuweka ndoa hatarini kutokana na michepuko ya kila mara,’’ alisema mpambe wetu.

Juzi mambo yalimwendea mrama akina mama wenye hasira walipoahidi kumpiga vita kwa kumnyima vibarua endapo angezuru makazi yao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.