Bodaboda aachwa kwa mataa kuhadaa kidosho

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale - Na Nicholas Cheruiyot

MWANABODABODA wa hapa aliachwa na demu wake alipogundua kwamba pikipiki aliyokuwa akiendesha haikuwa yake.

Semasema mtaani zaeleza polo alimrushia demu ndoano juzi na akameza chambo. “Nimejikaza hadi nikanunua bodaboda hii. Bila shaka nitakupa pesa uanze biashara upendayo hivi karibuni,” polo alimwambia demu na kungurumisha pikipiki kwa madoido.

Demu alimkubali lakini baada ya muda mfupi alibaini ukweli. Inasemekana kuwa siku ya tukio polo alikuwa amebeba demu kwa bodaboda mdosi alipowapata na kuwasimasha. Mdosi alizomea polo kwa kumhepa siku tatu mfululizo na kutompa mapato ya kila siku.

Baadaye demu aliambia marafiki alimtema polo kwa kumdanganya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.