Pasta pabaya kudai polo deni la Sh100 hadharani

Taifa Leo - - Dondoo! Za Hapa Na Pale -

PASTA mmoja kutoka mtaani hapa alijipata kona mbaya alipozomewa na kalameni kwa kudai deni lake kwa fujo mbele ya watu.

Duru zinasema jamaa alimkopa pasta Sh100 na akakawia kurudisha hadi akadhani pasta alikuwa amesahau. Hata hivyo mtumishi wa Mungu alikosa subira na akakata kauli kumdai jamaa mbele ya umma walipokutana mtaani. “Wewe ni mtu sampuli gani hata hauna shukrani baada ya kukukopesha pesa zangu. Nimechoka kusubiri ahadi zako za uongo,” alisema.

Yasemekana jamaa alimgeukia na kuanza kumfokea kwa kumuabisha mbele ya watu. “Hauna haya kuja kunizomea mbele ya watu na wewe ni mtumishi wa Mungu. Sitakulipa fanya utakalo,” jamaa alisema na kuondoka.

No John Musyoki

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.