Uchina yazindua tovuti ya kuripoti ujasusi dhidi yake

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia - Na Mashirika

UCHINA imeongeza kampeni yake dhidi ya shughuli za kijasusi zinazoendeshwa na baadhi ya watu na mashirika ya kigeni dhidi yake.

Kwenye juhudi hizo, taifa hilo limezindua tovuti maalum kwa lugha ya Mandarin na Kiingereza, ambapo inatoa wito kwa raia wake kuripoti habari zozote kuhusu vitendo wanaoshuku vinahatarisha usalama wa kitaifa.

Tovuti hiyo maalum ilizinduliwa na Wizara ya Usalama wa Ndani mnamo Jumapili.

Pia, serikali, kupitia tovuti hiyo imewaomba raia wake kuripoti kisa chochote ambapo afisa wa usalama atapatikana akichukua hongo.

Mkakati huo pia unawalenga raia wa kigeni ambao wanakutana na Mchina ambaye “anadaiwa kufanya kitendo chochote ambacho kimehatarisha usalama wa taifa.”

Kulingana na wachanganuzi, juhudi hizo ni sehemu ya serikali kuwakabili watu ambao wamekuwa wakiandaa vikao na wakosoaji wake.

Kulingana na kanuni zilizotolewa, wale ambao watatoa habari hizo muhimu kwa vikosi vya usalama watapewa zawadi nono. Hata hivyo, haikubainika mara moja zawadi ambayo itatolewa; ikiwa ni pesa au la.

Baadhi ya ripoti zilisema kuwa yule atakayetoa habari hizo atalipwa hadi Sh730,000.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.