Aliyeshukiwa kuua mke na mwanawe apatwa amefariki

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia - Na AFP

RAIA mmoja wa Korea Kusini ambaye anakabiliwa na tuhuma za mauaji ya mkewe na mwanawe mapema mwaka huu amefariki katika hali tatanishi, wamesema polisi.

Kim Min-ho, mwenye umri wa miaka 42, alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kuwaua wawili hao katika hoteli ya kifahari ya Ritzcarlton, mjini Hong Kong.

Taarifa zilisema kwamba mshukiwa alipatikana akiwa amepoteza fahamu katika gereza la Lai Chi Kok jana asubuhi, ila baadaye alitangazwa kufariki baada ya kufikishwa hospitalini.

Licha ya hayo, polisi hawakueleza bayana kilichopelekea kifo hicho, ila baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba alijinyonga.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.