Uturuki yakosoa dai la Macron kuhusu Syria

Taifa Leo - - Habari Za Afrika Na Dunia - Na AFP

UTURUKI jana ilimkosoa vikali Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kwa madai yake kwamba nchi hiyo ina uhusiano wa karibu na utawala wa Syria.

Mnamo wikendi, Bw Macron alidai kwamba mashambulio ya nchi za Magharibi dhidi ya utawala wa Rais Bashar al-assad wa Syria “umeifanya Uturuki kuwa karibu zaidi na Syria.

Lakini jana, Naibu Waziri Mkuu Bekir Bozdaf alisema kuwa sera na msimamo wa Uturuki kuihusu Syria ni huru, ila hauegemei upande wowote.

“Msimamo wetu kuhusu yanayoendelea Syria umekuwa huru. Hatujaegemea upande wowote, kama inavyodai Ufaransa. Msimamo wetu ni kwamba lazima kuwe na mwafaka utakaokubaliwa na pande zote mbili,” akasema kiongozi huyo, kwenye kikao na wanahabari.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.