Parklands wafyata ndimi zao mbele ya miamba KSG Ogopa

Taifa Leo - - Spoti - Na Patrick Kilavuka

KENYA School of Government (KSG) Ogopa, iliwalemea wenyeji Parklands SC kwa mabao 2-0 katika mchuano wake wa pili katika ligi ya FKF, Kauntindogo, tawi la Nairobi Magharibi, Jumapili. Victor Oloo alifunga bao la kwanza dakika ya 19 naye Serby Kivairo akaongeza dakika ya 38. Riruta United/makarios iliadhibu Kitisuru All Stars 2-1 katika mechi nyingine. Washindi waliongoza kipindi cha kwanza kupitia bao kujifunga la Josphat Wachira dakika ya 35 na Ford Ikutwa dakika ya 41. Kitisuru ilifuta machozi dakika ya 56 kupitia Fay Edward kipindi cha pili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.