Koriando wawabamiza Jomvu

Taifa Leo - - Spoti - Na Charles Ongadi

KORIANDO FC ililazimika kusubiri hadi kipindi cha pili ndipo ikailaza Jomvu Youth 2-0 katika mchuano wa ligi ya Mombasa Primia daraja ya pili uwanjani Shimo Annex, Jumapili. Timu zote mbili zilikosa nafasi nyingi za wazi katika kipindi cha kwanza. Kenedy Ngalla alifunga bao la kwanza katika dakika ya 85 baada ya kuwatoka walinzi wa Jomvu naye Albert Badi akapachika la pili dakika ya 89. Koriando, ambayo imekuwa ikishiriki ligi hii bila mkufunzi mkuu, nusura iongeze bao la tatu katika muda wa ziada, lakini kombora safi la Ngalla ilipanguliwa na kipa na kuwa kona ambayo haikuweza kuzalisha matunda.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.