Flash yazima Kali kwenye mpimano

Taifa Leo - - Spoti - Na Oscar Kakai

FLASH FC iliinyuka Kali FC 3-1 kwenye mechi ya kupimana nguvu iliyochezwa Jumapili katika Shule ya Msingi ya Kainuk. Mechi hii ya kusisimua ilianza kwa kasi huku Flash ikitangulia kuona lango dakika ya tisa kupitia kwa Evans Okibar. Bao la pili lilifungwa na Peter Nanok dakika ya 60 kabla ya Elias Ekadeli kuongeza bao la tatu wavuni dakika ya 64. Kali ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 80 kupitia kwa Joseph Lokwaro.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.