Beef wakaangwa bila bughdha kwao

Taifa Leo - - Spoti - Na Richard Maosi

BEEF Research ilikuwa na shughuli pevu kupenya lango la Greenbelt iliponyolewa 2-0 katika uwanja wa Pipeline katika mechi ya ligi ya FKF tawi la Nakuru ukanda wa kati, Jumapili. Wageni walikuwa mbele dakika ya 10 kupitia shuti kali la Julius Bii. Nathan Mwangi aliongeza bao la pili dakika ya 38 alipokamilisha krosi safi. Licha ya kuimarisha mashambulizi katika kipindi cha pili, Beef hawakupata bao. Kwingineko, Verona walitoka 1-1 na FC Basel. Wilfred Tenai na Samwel Ndiema waliona lango dakika ya 47 na 59.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.