Butali watoa tahadhari kali kwa mahasimu wao

Taifa Leo - - Spoti - Na JOHN KIMWERE

MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Magongo nchini Butali Warriors (wanaume) na Sliders (wanawake) walitia kapuni pointi tatu muhimu kila mmoja baada ya kushinda mechi zao uwanjani City Park jijini Nairobi, wikendi.

Butali, ambao ni wapinzani wakuu wa mabingwa watetezi Kenya Police, walibamiza mabingwa wa zamani Nairobi Simba 2-1 na kufungua kampeni yao vyema msimu huu. Sliders wanaojipanga kushiriki Klabu Bingwa Afrika baadaye mwaka huu, walipepeta Vikings 5-0 kwenye mchezo ulioegemea upande mmoja.

Vikings ilipokezwa kipigo hicho siku moja baada ya kuzoa alama moja ilipotoka sare ya 1-1 na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta. Sliders ilipata ufanisi huo kupitia mabao mawili ya Doris Kirui nao Nancy Kibogong, Christine Mbone na Anita Agunda walitikisa wavu mara moja.

Nahodha wa Butali, Kenneth Nyongesa alipongeza wachezaji wenzake kwa kufanya kazi nzuri iliyowasaidia kufungua msimu vyema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.