Bulemia na Nyuki waridhika na sare

Taifa Leo - - Spoti - Na Titus Maero

BULEMIA FC ililazimisha sare ya 1-1 dhidi ya wenjeji Nyuki Starlets FC katika Ligi ya Daraja ya kwanza ya wanawake ya Zoni B, Jumapili. Timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza bila kufungana bao uwanjani Ibinzo. Katika kipindi cha pili, Nyuki ya mkufunzi Edgar Akhonya ilichukua uongozi kupitia kwa Lucy Khameta katika dakika ya 74. Kiungo Patricia Apiyo alisawazishia Bulemia ya kocha Boniface Okumu dakika ya 85.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.