Rai vipusa wa ligi kuu wasicheze Chapa Dimba

Taifa Leo - - Spoti - Na Abdulrahman Sheriff

KOCHA wa Mombasa Olympic FC, Joseph Oyoo amependekeza wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya soka ya wanawake wasiruhusiwe kushiriki mashindano ya Chapa Dimba ama michezo baina ya kaunti.

Oyoo alisema wanasoka kutoka ligi kuu huwa tayari wameshajiendeleza na kushiriki kwenye mechi za Chapa Dimba na zile za kaunti kunawanyima wachezji chipukizi nafasi ya kuinua vipaji vyao.

“Ni muhimu Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) litoe sheria inazyozuia wachezaji wanaochezea timu za Ligi Kuu,” alisema.

Aidha, mkufunzi huyo alisema hawezi kulalamika kwa kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Mathare Ladies FC katika Ligi Kuu uwanjani wa Mbaraki.

Kulingana naye, matokeo hayo si ya kushangaza kwani walistahili kufungwa zaidi ya mabao hayo kwa sababu hawakuwa na wachezaji 11 wa kwanza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.