DIWANI ALIYEPIGWA MARUFUKU BUNGENI AOKOLEWA NA MAHAKAMA

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Barack Oduor

MWAKILISHI katika Bunge la Kaunti ya Homabay aliyepigwa marufuku ya miezi mitatu ya kutotia guu bungeni na faini ya Sh70,000 sasa ana sababu ya kufurahi baada ya mahakama kusitisha marufuku hiyo.

Joan Ogada ambaye ni Diwani wa Kojwach alipata adhabu hiyo Machi 13, 2018 baada ya kuvunja rungu la mamlaka wakati vurumai zilipozuka kuhusiana na kupitishwa kwa mojawapo ya sheria tata katika bunge hilo.

Kulingana na amri kutoka Mahakama ya Wafanyakazi ya Kisumu, usimamizi wa Kaunti ya Homabay umetakiwa umruhusu Bi Ogada aendelee kushiriki katika shughuli za bunge la kaunti.

Bi Ogada pia amewataka waliomchagua kutobabaika kwamba hatawahudumia vizuri akisema sasa mambo yote yatasalia kama kawaida wakisubiri uamuzi wa mwisho wa mahakama.

“Nawaomba wananchi kutoka wadi yangu kuwa watulivu na wenye subira japo kwa sasa nitawahudumia kama kawaida,” akasema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.