Nyota

Na Sheikh Khabib

Taifa Leo - - Fumbo & Falaki -

KONDOO

Machi 21- Aprili 20:

Miradi yoyote unayoifikiria kwa wakati huu haitakufaa hadi upate utaalamu kamili. Fuata ushauri utakaopewa kwa sababu hujiwezi peke yako ili usijute baadaye.

NG’OMBE

Aprili 21- Mei 20:

Hakuna kitu leo kwa watu wa nyota hii. Lengo lao kwa wakati huu ni kupata pesa za matumizi ambayo hayapunguziki. Naona nia ya kufanikiwa itakupa shida sana.

MAPACHA

Mei 21- Juni 21:

Walio na madeni yako wako katika nafasi nzuri ya kukulipa. Wapigie simu mara moja ili hali yako ya sasa ibadilike. Hatua hiyo itabadilisha maisha yako sana.

KAA

Juni 22- Julai 22:

Ni vyema kujaribu bahati kwingine ikiwa hali imekuwa ngumu sana. Uliyozoea kufanya kila siku si muhimu sana kwa sababu hayajakufaa kwa vyovyote.

SIMBA

Julai 23 - Agosti 22:

Ni siku nzuri na unashauriwa ufanye bidii kwenda madukani ama masokoni ukanunue bidhaa. Kumbuka zawadi. Hata zikiwa ndogo, kwa sababu zitabadilisha uhusiano wako na watu fulani.

MASHUKE

Agosti 23 - Septemba 23:

Usitarajie pesa zozote. Unazongoja zitachelewa kidogo na usipochukua hatua nyingine maisha yako yatakuwa magumu mno. Anza mipango mipya ili usitese wanaokutegemea.

MIZANI

Septemba 24 -Oktoba 23:

Kutoelewana na mtu wako kunatokana na mambo madogomadogo unayofanya ambayo yamekuwa yakimuudhi. Ikiwa unataka amani na raha kati yenu, jiepushe na mambo asiyopenda.

NGE

Oktoba 24 -Novemba 22:

Penzi lililokutoka linaweza kutokea tena na kukuletea furaha katika maisha yako. Hata hivyo, kwanza suluhisha yaliyolitorosha. Elewa hatari zinaweza kutokea usipowajibika.

MSHALE

Novemba 23 -Desemba 21:

Hata ukiwa na tahadhari kiasi gani, leo utachezewa shere. Chunga usipoteze pesa zako katika mambo yasiyo na manufaa. Usianzishe mradi wowote mpya wakati huu hasa na wageni.

MBUZI

Desemba 22 - Januari 20:

Utakuwa na bahati kupata unachotafuta kwa wakati huu. Kwa hivyo, jiandae kushughulikia bahati hiyo ili furaha isikuzidi. Lakini usikubali watu wajue unatarajia mazuri wazizime mazuri yako.

NDOO

Januari 21 - Februari 19:

Bahati mbaya iliyokufika hivi majuzi ilitokana na uzembe wako kimapenzi. Ulianguka mtihani, lakini huo si mwisho wa maisha. Jirekebishe, utubu makosa yako kisha umrudie.

SAMAKI

Februari 20 -Machi 20:

Usishangae kuona mambo yakikwendea kombo wakati huu. Mpango wako wa maisha hautafanikiwa hivi karibuni lakini utafika unapotaka hatimaye. Stahamala ni muhimu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.