Sifa, uundaji wa misimu katika Kiswahili

Taifa Leo - - Ukumbi Wa Lugha Na Fasihi - MARY WANGARI

Katika makala ya leo tutaangazia dhana, dhima na nafasi ya misimu katika lugha ya Kiswahili.

Misimu ni lugha ya kisirisiri yenye mafumbo ambayo hutumiwa na kundi dogo la watu katika jamii.

Ni usemi wa muda tu na hutoweka baada ya muda mfupi na yale yanayobaki husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha inayohusika.

Sifa za misimu

Misimu huzuka na kutoweka. Baadhi ya hubadilika na mingine hudumu na kuingizwa katika lugha inayohusika.

Ni lugha isiyokuwa sanifu. Maneno ya misimu mara nyingi huzushwana watu kutokana na hali zinazowapata kwa wakati huo.

Haifahamiki na watu wasio wa kundi hilo. Ni lugha ya mafumbo.

Wakati mwingine hubadilika na kuwa sehemu ya msamiati wa lugha husika. Huweza kupotea na kufa.

Misimu huwa na chuku nyingi. Maneno mengi ya misimu huwa yanakejeli na yenye kutiwa chumvi.

Zinaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Neno la misimu linalotumiwa sehemu moja linaweza kuwa na maana tofauti na lina-vyotumikamahali pengine.

Misimu huhifadhi historia ya jamii hasa kuhusu maendeleo ya lugha (hasa pale inapoishia hata kukubaliwa katika lugha fulani)

Hupendeza sana miongoni mwa watumiaji wake. Hii ni kwa sababuina mvuto mkubwa.

Wazee wakitumia misimu aina ya Sheng’ huonekana kama watovu wanidhamu. Jinsi ya kuunda misimu 1.Kuchanganya maneno ya lugha tofauti. Kwa mfano: Niliwahi bob.

2. Kwa kuchanganya maneno kisha kuyasongoa.

Kwa mfano: Mother –masa.

3. Kutafsiri kijuujuu. Kisisisi. Kwa mfano: Kugo.

4. Kwa kutumia sauti za tanakali. Kwa mfano: Mtutu – bunduki (kutokana na mlio wake)

5. Kwa kutumia sitiari, Kwa mfano: Ngoma – Ukimwi, golikipa – nyani. 6. Kufupisha maneno, kwa mfano, komputa –komp

Kutokana na maneno ya kigeni, kwa mfano father kuwa fathe, head kuwa hedi 7. Maneno kupewa maana mapya. Kwa mfano, Chuma –gari mpya.

Sababu ya kutumia misimu

1. Hutumiwa kwa ajili ya kutaka mazungumzo yawe siri; yasieleweke kwa watu wengine.

2. Hutumiwa ili kufanya mambo mazito kuwa mepesi.

Kwa mfano, mtu anapokusaidia kutenda jambo na atake kuhongwa anaweza kukuuliza,‘’ndugu, hakuna hata chai?’ badala ya kukuuliza,’’ndugu, mbonahunipi hongo?’’

3. Kudhania kuwa matumizi ya misimu ndio ujuzi wa lugha.

Kutojua lugha moja vizuri. Kwa mfano, wasemaji wengi hawajui Kiswahili wala Kiingereza vyema.

4. Ni kama uraibu kwa vijana.

Misimu hurahisisha mawasiliano. Maneno ya misimu hueleweka kwaharaka, hasa yanapotumika badala ya maelezo mengi.

5. Hutumiwa kama tauria au tasifida. Kuna baadhi ya misimu ambayohupunguza ukali wa maneno hasa lugha ile inayoonekana ya matusi.kwa mfano: kukeketa mabinti badala ya kutahiri mabinti.

6. Misimu huunganisha watu.

Watu wa matabaka mbalimbaliwanapokuwa katika mazungumzo huelewana vyema wanapotumia lugha wanayofahamiana.

7. Misimu mingine huikosoa na kuiasa jamii.

Misimu ya namna hii huwana hisia zakejeli, bezo, dhihaka, chuki na kusifu kusiko kwa kawaida.

8. Misimu huibua hisia za wazungumzaji na hata wasikilizaji.

Mara nyingi misimu hubeba hisia za furaha, huzuni, chuki, mshangao,mzubao miongoni mwa hisia nyingine.

9. Misimu huikosoa na kuiasa jamii. Misimu ya namna hii huwa na hisia za kejeli, bezo, dhihaka, chuki na kusifu kusiko kwa kawaida.

10. Misimu hufurahisha na kuchekesha. Hii ni kwa kwa sababu maneno yamisimu yana mvuto na kuwa na chuku yanapotumiwa na kuchekesha.

“Hutumiwa ili kufanya mambo mazito kuwa mepesi”

marya.wangari@gmail.com

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.