Washukiwa 3 zaidi washtakiwa kwa kushambulia mfanyibiashara

Taifa Leo - - Front Page - Na BERNARDINE MUTANU

IDADI ya watu wanaokufa kutokana na ajali za barabarani imepungua mwaka huu, lakini ajali hizo bado zingali jinamizi.

Shirika la Kitaifa la Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA), jana lilisema kuna haja ya kutafuta mbinu za kuhakikisha hakuna hata mtu mmoja anayefariki ajalini nchini.

Kutokana na utafiti, watu wanane hadi 10 hufa kila siku maeneo tofauti nchini kutokana na ajali za barabarani, alisema Bi Njeri Waithaka, Mkurugenzi wa Usalama Barabarani wa NTSA.

“Idadi ya vifo imepungua kwa asilimia 3.9 pekee. Hata hivyo hatufai kumpoteza mtu hata mmoja,” alisema Afisa Mkuu wa Usalama na Mikakati wa NTSA, Dkt Kibogong wakati wa mkutano na wanahabari, baada ya kuzindua warsha ya washikadau katika Chuo Kikuu cha Strathmore, Nairobi.

Kulingana na NTSA, kati ya Januari 2018 na Mei 14, watu 1,095 walikuwa wameaga dunia baada ya kuhusika katika ajali za barabarani, ikilinganishwa na watu 1,139 walioaga dunia katika kipindi hicho mwaka jana.

Pia, idadi ya watu waliohusika katika ajali ilipungua hadi 4,193 kutoka 4,676 kipindi hicho mwaka jana.

Kulingana na Dkt Kibogong, thamani ya watu walioaga dunia ni zaidi ya Sh350 bilioni kwa mwaka, ambayo ni asilimia tano ya jumla ya mapato ya Kenya.

Alisema idadi kubwa ya wanaoaga dunia katika ajali za barabarani ni watu wanaotembea kwa miguu na vijana kati ya miaka 24 na 34.

Katika kipindi hicho, watu 427 waliaga dunia baada ya kuhusika katika ajali barabarani wakitembea kwa miguu, na kufuatwa na abiria (224) na wanaoendesha pikipiki (213).

Licha ya kuwa dogo, eneo la Nairobi liliripoti visa vingi zaidi (400), alisema mkurugenzi huyo.

Bi Waithaka alisema kuna haja ya kushirikisha mashirika ya utafiti kwa lengo la kupunguza idadi ya vifo barabarani kwa asilimia 50 kufikia 2020.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.