Waislamu waomba bei ya vyakula ishushwe

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Kalume Kazungu

wa dini ya Kiislamu kaunti ya Lamu wameiomba Serikali kushukisha bei ya bidhaa, hasa chakula msimu huu wa Ramadhan.

Wakizungumza na Taifa Leo kisiwani Lamu jana, walisema bei ya vyakula ni ya juu mno na wanataraji serikali kuwahurumia na kushusha bei za vyakula, hasa tende.

“Tunafurahia ujio wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Ombi letu kwa serikali, hasa Rais Uhuru Kenyatta ni kwamba, bei za vyakula zishushwe. Tutafurahia ikiwa tende, unga, mchele, viazi na vinginevyo vitashukishwa bei msimu huu wote wa Ramadhan,” akasema Bw Hassan Chonda.

Waumini hao pia wamewataka Wakenya kuutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kusameheana wao kwa wao ili kuziba makovu yaliyochangiwa na siasa na kampeni za uchaguzi uliopita wa Agosti 8. Bw Muhashiam Famau pia aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuutumia Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuombea amani na umoja kuzidi kudumu miongoni mwa Wakenya hapa nchini na ulimwenguni.“tunapoadhimi sha Ramadhan, huu ni wakati wa wakenya kuja pamoja. Wazike tofauti zao na kusahau siasa za Agosti 8,”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.