Shollei ajitetea dhidi ya madai ya kukosa kuhudumia wananchi

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na Wycliff Kipsang

MWAKILISHI wa Wanawake katika Kaunti ya Uasin Gishu Gladys Boss Shollei jana alikanusha madai kwamba amewasahau wakazi wa kaunti hiyo.

Bi Shollei hajakuwa akionekana hadharani kwa muda, hali ambayo imezua hisia mseto miongoni mwa wakazi.

Lakini jana, kiongozi huyo alipuuzilia mbali wanaomkosoa, akisema amekuwa akiendesha shughuli za kuwahudumia wananchi kichinichini.

“Nimekuwa nikitangamana na wananchi, hasa wanaokabiliwa na changamoto za kiuchumi katika jamii. Hiyo ndiyo kazi yangu. Si lazima nionekane hadharani. Huu ni wakati wangu kuwahudumia wananchi,” akasema.

Baadhi ya viongozi ambao wamemkosoa ni Mbunge wa Kapseret, Oscar Sudi, ambaye amekuwa akimlaumu kwa madai ya kuwasahau wakazi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.