Mishi ashauri wakazi kufuata mwongozo wa Joho

Taifa Leo - - Habari Za Kaunti - Na HAMISI NGOWA

MBUNGE wa Likoni, Mishi Mboko amewataka wakazi wa Pwani kufuata mwelekeo wa kisiasa utakaochukuliwa na Gavana wa Mombasa, Ali Hassan Joho ili kuhakikisha wanakuwa ndani ya serikali ijayo baada ya hatamu ya Rais Kenyatta kukamilika.

Akizungumza katika eneo la Mtongwe, Bi Mboko alisema Bw Joho ndiye kiongozi anayetambulika zaidi kwa utetezi wa maslahi ya Wapwani na akamtaja kama anayetosha kutoa mwongozo kuhusu mustakabali wa siasa za eneo hilo katika uchaguzi ujao.

Alisema wakazi wa Pwani kamwe hawatakubali kutumiwa na viongozi wengine kama ngazi ya kufikia malengo yao akisisitiza kwamba lazima watambuliwe na kujumuishwa vilivyo katika serikali.

“Nafahamu tayari wengine wameanza mazungumzo ya kupanga mikakati ya 2022 lakini sisi kama Wapwani tunasema tutakuwa kwa mazungumzo yatakayokuwa na manufaa kwetu na ambayo yatamtambua Joho kama kinara wetu,” akasema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Kenya

© PressReader. All rights reserved.